Timothy Marko.
Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam limewakamata vijana wa kikundi kinacho shughulika na uhalifu jijini Dar es salaam maarufu kama mbwa mwitu kufuatia hofu iliyotanda katika jiji hilo kuhusiana na kikundi hicho.
Akizungumza jijini leo kamishina wa polisi wa kandamalum Dar es salaam Suleiman kova amesema kuwa jeshi lake limewa wakamata vijana 155 ambao hujishughulisha na vitendo vya uhalifu ikiwemo uporaji ,uvutaji wa madawa ya kulevya .
‘’jeshi la polisi lime wakamta vijana takribani 155 wanaoji ita mbwa mwitu kufuatia operesheni iliyofanywa katika mikoa maalumu yakipolisi ambapo tumegundua kundi hili linajihusisha pia nauvutaji wa madawa yakulevya ikiwemo bangi pamoja na kubeli’’alisema kamanda Suileiman Kova .
Kamanda Kova alisema kuwa licha ya kujihusisha na uvutaji wa madawa yakulevya pia kundi hilo hushiriki katika ngoma za usiku maarufu ‘’vigodolo’’ambapo huji hushisha vitendo vya kiharifu wakati wangoma ya aina hiyo pindi inapo chezwa nyakati za usiku .
Alisema katika kuhakikisha kundi hilo linatokomezwa kabisa jeshi lake liliamua kufanya msako maalumu katika maeneo ya magomeni ,kigogo,Tabata ,Mbagala na maeneo yote yanayozunga mto msimbazi aliongeza kuwa bado jeshi lake lina endelea na operesheni hiyo ilikuhakikisha vikundi vya aina hiyo haviibuki tena.
‘’maeneo yaliyo athirika navikundi hivi nipamoja na kigogo,Magomeni, Tabata Mbagala pamoja na maeneo yanayozunguka mto msimbazi’’aliongeza kamanda kova.
Aliongeza kuwa baada yamsako huo ulliofanywa na polisi walibaini kuwa kundi hilo linaongozwa Athuman Saidi (20) mkazi wa kigogo ambapo mtuhumiwa huyo alikiri kuongoza kundi za idi ya watu 15 ambao baadhi yao nikati yawaliokamatwa .
Alisisitiza kuwa baadhi yakikundi hicho hujihusisha na ngoma kama vigodolo ,mchiriku ,kangamoja nakuongeza kuwa baada yakutoka kwenye ngoma hizo hujihusisha nahalifu.
‘’tunawasiliana na maafisa utamaduni wa wilaya zote za mkoa wa Dar es salaam kuasimamisha utoaji vibali wa ngoma za usiku ambazo hazina tija’’alisisitiza kamanda Kova.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni