Timothy Marko.
Kituo cha haki nasheria za binadamu nchini (LHRC)kimebaini kuwa baadhi vyama vya siasa vimekuwa vikitumia lugha zisizo za staha zenye kashifa ndani yake na kejeli katika uchaguzi mdogo katika jimbo la chalinze ambapo vyama hivyo vilitumia lugha hizo ilikunadi sera zake kwa wananchi.
Akitoa tathimini hiyo hii leo jijini ,mratibu wa kituo hicho Martina kabisama amesema matumizi ya lugha zisizo za staa zilitumika katika vyama vya CUF,CHADEMA,CCM,ambapo alibaini nisha moja ya kejeli ambazo zilitumika kunadi vyama vyao kwa wananchi kama’’ mtoto huyu si riziki’’kama ilivyotumiwa na chadema kwa katibu wa CCM na katibu wa chamahicho cha CCM kujibu mapigo kuwa kumjibu na kumdhihaki kuwa hajaenda jando.
‘’Makamu mwenyekiti wa chadema alimtuhumu katibu mwenyenezi wa CCM kuwa ‘’huyu mtoto si riziki ‘’ Katika mkutano wa kufunga kampeni uliofanyika chalinze sokoni tarehe 5/4/2014 akiwa anajibu kejeli za katibu mwenezi wa CCM,Nape nauye ambaye katika moja yamikutano ya kampeni alisikika akimdhihaki mgombea wa chadema kwamba haja enda jando’’alisema Martina Kabisama.
Martina kabisana alisema kuwa kumekuwepo nanyimbo zinazo eneza chuki dhidi ya vyama vingine mfano nyimbo za CCM zilikuwa zina hamasisha chuki na uchochezi kama alama za vidole viwili inayotumiwa na CHADEMA kuwa ni alama ya FREE MASON nakusema kwamba ukijiunga na chedema utakuwa umejiunga na free mason .
Alisema katika uchaguzi mdogo wa chalize kumekuwa na mwitikio mdogo wa jimbo la chalinze ambapo idadi ya wapigakura ilishuka kutoka wananchi 92,939waliojiandikisha hadi kufikia wananchi 24,422 waliojitokeza kupiga kura sawa na asilimia 26.3 ya wapiga kura wote waliojitokeza kwenye uchaguzi huo .
‘’Tumebainikuwa moja ya changamoto zakutoboreshwa kwa daftari la kupigia kura nakutoandikishwa kwa wapigakura wapya hivyo kundi kubwa la vijana kuachwa nje kwenye uchaguzi huo timu ya waangalizi ilishuhudia vijana wengi walijitokeza katika kampeni za wagombea lakini siku yakupigaji wa kura hawakujitokeza kabisa nakatika mahojiano walikiri kuwa wakupiga kura kutokana nakuto andikishwa kwa daftari lakupigia kura’’aliongeza mratibu wa taifa Martina Kabisana.
Mratibu wa taifa aliongeza kuwa kume kuwa namaandalizi duni kwenye baadhi yavyama vitano ambavyo ni AFP,CCM,CHADEMA, CUF,NRA ambapo sheria ya uchaguzi inawatataka vyama vyasiasa kuwasilisha msimamizi wa uchaguzi ratiba yamikutano yao ya kampeni kabla yakuanza kampeni zao nakubainishakuwa vyama vyote vilitii agizo hilo isipo kuwa hawakuweza kuhudhuria mikutano yote,
Aliongeza kuwa kume kuwa naukosekanaji wa uwazi katika tume ya uchaguzi ambapo tume yauchaguzi ilitoa taarifa yauboreshwaji na uhakiki wawapigakura bila yakuwashirikisha wadau wawa piga kura ambao ni vyama vya siasa katika taarifayake ilionyesha iliongeza wapigakura wapatao 80 nakuboresha idadi yawapigakura wengine.
‘’ kituo cha msoga shule yamsingi no1.Mzee idd Halfan kizigo na bi Khadija Omary Selemani walikuwa na kadi lakini majina yao hayakuwepo kwenye Dafutari lakupigia kura licha yaorodha kubandikwa ‘’alisema mratibu huyo wa taifa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni